RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AMTEUA DKT. TULIA ACKSON MWANSASU KUWA MBUNGE

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah anapenda kuufahamisha umma kuwa amepokea uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wa kumteua Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uteuzi huu ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 66( 1 )( e ) ambayo inampa madaraka Mhe. Rais kuteua Wabunge wasiozidi kumi ( 10 ).

Mhe. Tulia anakuwa Mbunge wa kwanza wa kuteuliwa na Rais na anatarajiwa kuapishwa katika mkutano wa kwanza wa Bunge la kumi na moja unaoanza kesho jumanne  tarehe 17 hadi 20 Novemba, 2015.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dodoma,
16 Novemba, 2015

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni