BARCELONA, CHELSEA NA BAYERN MUNICH ZAFANYA MAUAJI UEFA

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Barcelona wametinga rasmi hatua ya mtoano baada ya kuichakaza AS Roma kwa mabao 6-1 huku ikishuhudia nyota wake Lionel Messi na Luis Suarez wakifunga mabao mawili kila mmoja na Jordi Alba na Adriano Correia wakifunga bao moja kila mmoja.


Katika mechi nyingine ya kundi hilo Bate Borislov ikatoka sare na Bayer 04 Leverkusen ya bao 1-1, Arsenal ikafufua matumaini ya kufuzu baada ya kuicharaza Dinamo Zagreb mabao 3-0 shukrani kwa mabao ya Alex Sanchez aliyefunga mara mbili na Mesut Ozili bao moja. 

Bayern Munich nayo ikajiakikishia kutinga 16 bora baada ya kuichabanga Olimpiacos mabao 4-0 yaliyofungwa na Douglas Costa, Roberto Lewandowski,Thomas Muller na Coeman.

Zenit St Petersburg ikajihakikishia kumaliza kinara wa kundi lake kwa kuizima Valencia mabao 2-0 nayo Gent ikishinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya Olimpic Lyon. 
FC Porto ya Ureno ikajikuta inakwama nyumbani kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Dinamo Kiev nayo Chelsea ikashinda ugenini kwa bao 4-0 dhidi ya Macabi Tel Aviv.

MLIPUKO ULIOLILENGA BASI LA WALINZI WA RAIS TUNISIA WAUWA WATU 12

Mlipuko umelilenga basi lililokuwa limebeba walinzi wa rais katika Jiji la Tunis nchini Tunisia na kuuwa watu 12.

Kufuatia tukio hilo rais Beji Caid Essebsi ametangaza siku 30 za hali ya hatari na kutangaza watu kutotembea ovyo katika Jiji la Tunis.

Tunisia imekuwa ikikapiliwa na mashambulizi ya kundi la Dola ya Kiislam (IS), likiwemo tukio la mtu mwenye silaha kuwashambulia watu kwenye hoteli ya ufukweni ya Sousse mwezi Juni na kuuwa watu 38.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni