UZINDUZI WA USHIRIKA WA MAMA NA BABA LISHE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 15, 2015

Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya Ya Mama na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Said Said (wa pili toka kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam. Lengo la jumuiya hiyo kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali, kutoa fursa kulinda haki za ajira na kuzitafutia ufumbuzi na kuondoa tatizo la ajira kupitia tasnia hii ikiwa ni kumtambua mama na baba lishe kama sehemu ya maisha ya kila mmoja wetu, kwani kila mtanzania anaufahamu umuhimu wa mama na baba lishe na takwimu zinaonyesha asilimia 50% ya wanzania waishio mijini hupata huduma ya chakula. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Mhonzu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Mama Lishe wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Waaandishi wa habari wakufuatia mkutano huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni