Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi
wa Msama Promotions, Alex Msama, alisema wameamua kuua ndege wawili kwa jiwe
moja, kwani sasa litafanyika Desemba 25, likibeba Sikukuu ya Krismasi na
shukrani hiyo ya kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu.
Alisema kutokana na tamasha hilo kubeba ajenda hizo mbili kwa pamoja, kamati yake imelipa uzito mkubwa kwa upande wa suala la maandalizi ambapo wameanza kuzungumza na waimbaji nguli wa kitaifa na kimataifa.
Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, litahamia katika mikoa mbalimbali itakayoteuliwa na kamati yake kwa kuzingatia kigezo cha wingi wa maombi na uwezo wao kifedha.
“Naomba ifahamike, tamasha hili la kumshukuru Mungu kuiwezesha nchi kuvuka salama katika mtihani mgumu wa Uchaguzi Mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa, litafanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,” alisema Msama na kuongeza:
“Unaweza kuona ni tamasha ambalo safari hii litakuwa na
uzito mkubwa, kwani litakuwa limebeba uzito wa Krismasi itakayoambatana na
shukrani maalumu kwa Mungu kutokana na kuijalia nchi kuvuka salama katika
Uchaguzi Mkuu,” alisisitiza Msama.
Kuhusu waimbaji, Msama alisema kamati yake itajitahidi
kuwaleta wenye uzito na mvuto kulingana
na uzito wa tamasha hilo, akiamini litakuwa na mvuto wa tofauti na
yaliyotangulia na kuwasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili kukakaa
mkao wa kupokea baraka za Mungu.
Msama kupitia Kampuni yake ya Msama Promotions, amechangia
kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Injili nchini kupitia ubunifu wake wa
kuratibu matukio ya muziki huo kuanzia tamasha la Pasaka, Krismasi na uzinduzi
wa kazi za waimbaji mbalimbali.
Juhudi hizo za Msama ndizo zimeufanya muziki wa Injili
kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kiasi cha kuwa moja ya ajira
kwa vijana wenye vipaji na karama ya kumtumikia Mungu kwa njia hiyo ua uimbaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni