Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ Estha Chaburuma
‘Lunyamila’ ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya
Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya
wanawake ya Malawi utakaochezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Azam
Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Chaburuma amekua ni
miongoni mwa wachezaji waanzilishi wa Twiga Stars ambapo amekua
akiitumikia timu hiyo tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa timu
inapojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma amesema wameamua kutumia mchezo
huo wa kirafiki kwa ajili ya kumuaga Chabruma ambaye amekua ni chachu ya
maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake, kutokana na kuwafanya
wanawake wengi kujitokeza kucheza mchezo huo.
Naye kocha wa timu
hiyo, Rogasian Kaijage amesema vijana wake wapo katika hali nzuri,
wananadelea na maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi, ambapo anaimani
watautumia vizuri katika kumuaga mchezaji mwenzao wa siku nyingi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni