Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku tatu.’
Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akiongea na waandish wa habari katika cliniki
iliyoanza tarehe 11 na kuendelea mpaka tarehe 13 katika hospitali ya Hindumandal
Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa utiwa mgongo na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad
akiongea na waandishi wa habari katika Klinik hiyo.
Shamila Idd mama wa mtoto Zulea mwenye tatizo la uti wa mgongo akiongea na waandishi wa habari katika kliniki iliyoandaliwa na Dr Alok Ranjan,
mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo.
Inakadiriwa kuwa
watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa
fahamu hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa
matibabu.
Kutokana na
hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini
daktari bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye
pia ni Mkuu wa idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali
hiyo DKT ALOK RANJAN ambaye atakuwa akitoa huduma na kuwaona wagonjwa
wake aliowafanyia upasuaji siku za nyuma.
Nao
baadhi ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika
hospitali ya hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali
kuhakikisha kwamba inasaidia katika gharama za matibabu ya watu
wanaosafiri nje ya nchi kufuata matibabu ya magonjwa mbali mbali.
Wamezitaka pia
kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za
kimataifa badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
Katika
mkutano huo na waandishi wa habari ulofanyika tarehe 12 katika
hospitali ya hindumandali Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali za Apollo
amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa maisha ili kuepukana
na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na sababu nyinginezo.
na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na sababu nyinginezo.
Tanzania kwa
sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa
sasa ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni