Wavuta sigara, wamiliki magari na
boda boda pamoja na wanaopenda kunywa juisi za viwandani nchini
Kenya, watasherehekea krismasi vibaya kutokana na ongezeko la kodi
linalotarajiwa kuwakabili.
Watumiaji wa bidhaa hizo watalipa
kodi zaidi baada ya rais Uhuru Kenyatta kuridhia muswada wa kodi wa
mwaka 2015, ikiwa ni jitihada za kuendelea kuwakamua wananchi kodi
ili kukabiliana na uhaba wafedha unaoikabili serikali.
Serikali ya Kenya kwa mara ya kwanza
mwaka huu imeongeza kodi kwa bidhaa ambazo kwa kawaida huchukuliwa
kama si za anasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni