Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akiwaeleza waandishi wa habari
(Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika
kufanya mikutano kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano ya (Video
comference) ambapo kikao kimoja kitawaunganisha pamoja washiriki kutoka
Mikoa 8 ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa
moja (interactivity) kwa maswali na ufafanuzi leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi
Kawawa.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa akifafanua
jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari
uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA
katika kufanya mikutano ambapo mfumo wa Mawasiliano ya (Video
comference) utatumika ili kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za
Serikali.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
Habari kuhusu faida za kutumia TEHAMA ikiwemo kuokoa fedha zilizokuwa
zinatumika awali kuandaa mikutano hiyo ambapo kwa sasa washiriki
watashiriki mikutano hiyo wakiwa katika vituo vyao vya kazi leo jijini
Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Uanzishaji
wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini
utaboresha na kuongeza ufanisi wenye tija ambao utapunguza gharama za
utendaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kupitia
utaratibu huu wa vikao kazi ambavyo vitaendeshwa kwa kutumia mfumo wa
mawasiliano ya video ambapo kikao kimoja kitaunganisha kwa pamoja
washiriki kutoka mikoa nane ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya
kuwasiliana moja kwa moja kwa maswali na ufafanuzi.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kupunguza gharama
za uendeshaji vikao kazi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni