PAPA FRANCIS AWASILI NCHINI KENYA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo jioni.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewasili jijini Nairobi nchini Kenya leo jioni tayari kwa ziara ya siku tatu nchini humo.

Alipotua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ( JKIA ), kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani alilalkiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.

Ziara ya Papa Francis nchini Kenya ni mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika itakayomchukua pia hadi nchini Uganda na baadaye Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni