Afisa Mtendaji Mkuu wa iliyokuwa NIKO Insurance Bw. Manasseh Kawoloka
akizungumza mbele ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya kubadilisha
jina la kampuni hiyo ambapo sasa inaitwa Sanlam General Insurance.hafla
hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Kampuni
ya Bima Niko Insurance limited Imebadili jina na kuwa Sanlam General
Insurance Limited.Mabadiliko hayo yanalenga Kupanua Wigo Na kuimarisha
uwepo wake Nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa Jumla.Sanlam General
Insurance Itaendelea Kutoa Huduma Mbalimbali za Bima Kwa Wateja Binafsi
na Mashirika Nchini Tanzania.Huduma za Sanlam General Insuarance ni
Pamoja na za Biashara na Binafsi kama vile Magari,Moto Na Nyinginezo.
Afisa
Mwandamizi wa Ukuaji wa Mashirika wa Sanlam Emerging Markets (SEM)
Ndugu Manasseh Kawaloka Akitoa Hotuba yake Kwenye halfa ya Kampuni ya
NIKO Insuarance Limited Ilipobadili Jina na kuwa Sanlam General
Insurance.Sanlam
General Insurance Yenye Makao Makuu yake Nchini Afrika KusiniInamiliki
46%ya Hisa za Niko.Kupitia Kampuni yake Tanzu ya Masoko yanayokua yaani
Sanlam Emerging Markerts..
Picha
ya Viongozi wa Kampuni ya Sanlan Pamoja na NIKO Insurance wakiwa
wameshikana mikono Mara baada ya Uzinduzi wa Sanlam General Insuarence.
Afisa
Mwandamizi wa Ukuaji wa Mashirika wa Sanlam Emerging Markets (SEM)
Alisema Kuwa Sanlam Group ni Kampuni yenye Sifa Kubwa,Hivyo Mabadiliko
ya NIKO Insurance Kuwa Sanlam General Insurance Utaleta Ufanisi wa Hali
ya Juu Pamoja Utendaji wa Kibiashara Kwa Kampuni Hiyo.Akieleza zaidi
alisema Watanzania sasa watapata nafasi zaidi ya Kupata Aina mbalimbali
za Bidhaa za Bima Zenye ubunifu kufidia Majanga Binafsi na ya
Kibiashara .
Kampuni
ya Iliyobadili Jina Sanlam General Insurance Inatoa Huduma Mbalimbali
za Bima Katika Wigo Mpana Kwa Wateja Binafsi Pamoja na Mashirika
Nchini Tanzania .Huduma Zitolewazo na Kampuni ya Bima ya Sanlam General
Insurance Zinalenga Biashara na Watu Binafsi Kama Magari ,Moto
,Uhandisi pamoja na Bima Maalum.Kabla ya Kubadili Jina Kampuni ya NIKO
Insurance Imekuwa Ikitoa Huduma Nchini Tangu Mwaka 2005.
Mjumbe wa Bodi ya Sanlam General Insurance (zamani NIKO Insurance)Ndugu Josep Mungai Akitoa Hotuba yake wakati wa Uzinduzi huo.
Mabadiliko
ya NIKO Insurance Limited kuwa Sanlam General Insurance Yanafuatia
Mabadiliko ya Kampuni ya African Life Assuarence ya Tanzania na Kuwa
Sanlam Life Insurance.Sanlam General Insurance Inatoa utaalamu na
Uzoefu wa Hali ya Juu kwa Wateja wake Pamoja na Wadua wengine wanaofanya
kazi na Kampuni hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni