Benki
ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika
tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo <b>Dk Muhsin Masoud alitoa
zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama
ioneshavyo pichani.
Mkurugenzi
huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini hapo ili
kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha
huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini.
Kilele
hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya
benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na
Main, vile vile Arusha na Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni