Mollel
ameyasema hayo wakati alipokuwa akijitambulisha na kuomba kura kwa wakazi wa
kata ya Levolosi na kuwataka kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi pamoja na yeye
kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha Mjini.
Alisema kuwa
anaomba kura kwa wanachama na wasiokuwa wanachama kwani maendeleo hayana
itikadi za vyama vya siasa hivyo akawataka kumtuma naye awe mtumishi wa
wananchi wa jimbo la Arusha mjini
“Mnajua
siendi kuganga njaa bungeni bali naenda kupeleka kero zenu na nani uchungu na
maendeleo ya kinamama,wazee na vijana kwani nitaanzisha saccos kwa kila kata
ilimpate mikopo ya kujikwamua na kuweza kujiletea maendeleo”alisema Mollel.
Aliwataka
wakereketwa na wale wafuasi wa vyama vingine kuweka pembeni ushabiki na
kumchagua yeye ilikuirudiisha Arusha kuwa Giniva ya Afrika na kuirudisha Arusha
yenye amani na kuweza kurudisha sifa ya jiji hilo.
Awali
akimkaribisha Mgombea kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho sanjari na
wananchi Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha Dkta Wilfred ole Soiley
amewakata kuacha ushabiki wa kisiasa na kumchagua Mollel kwani anatosha
kuongoza jimbo la Arusha.
Soiley
alisema kuwa pamoja na kupigwa katika uchaguzi mkuu kwa nafasi za udiwani mda
umefika kwani uchaguzi ulipita na sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kumpa
kura za kishindo mgombea wa chama hicho.
“Nawasihi
nduguzangu kutafuta wanachama kumi kwa kila mtu
ilikuunganisha nguvu na kuipa
ccm ubunge wa jimbo letu kwani nyinyi ni mashahidi wakubwa hakuna
kilichofanyika kwa mda wa mbunge aliyemaliza mda wake kwa kipindi cha miaka
mitano”alisema Soiley.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni