RAIS WA MISRI ABDUL FATAH AL-SISI ASEMA NI PROPAGANDA TU MADAI YA IS KUTUNGUA NDEGE

Rais wa Misri Abdul Fatah al-Sisi ameelezea madai kuwa wapiganaji wenye uhusiano na Dola ya Kiislam (IS) wameiangusha ndege ya Urusi ni propaganda tu.

Rais al-Sisi ameviambia vyombo vya habari kuwa ni mapema mno kuelezea kilichotokea kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo ikiwa na abiria wengi raia wa Urusi ilianguka penisula ya Sinai siku ya jumamosi na kuua abiria wote 224.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni