MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MUSONYE


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamau za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Theresia Musonye kilichotokea jana asubuhi katika mji wa Kakamega nchini Kenya.

Katika salamu zake, Malinzi amempa pole Musonye na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na watanzania wote, wako pamoja nae katika kipindi hiki cha kigumu cha maombelezo na kuwapa pole ndugu,jamaa na wafiwa wote.

Bi Theresia Musonye amefariki akiwa na umri wa miaka 77, taarifa zaidi na taratibu za mazishi zitatolewa na familia ya marehemu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni