Katika
kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji uwanja KADCO, mkuu wa
mkoa ameupongeza uongozi kwa kuongeza ndege zinazotua na kuruka, uwezo
wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na uwezo wa kudhibiti vitendo
haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji nyara za serikali na ugaidi.
Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza yafuatayo yatekelezwe;
1.
Uwanja wa Kia usiwe njia ya wapitishaji ea madawa ya kulevya kwani
kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana
2. Uwanja wa Kia usiwe njia ya kutorosha nyara za taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za taifa
3.
Ameagiza menejimenti kuutangaza uwanja huo kimataifa ili uvutie wageni
zaidi kuja kuona vivutio vya utalii tukivyonavyo na kufanya hivyo ni
kuongeza pato la taifa
Aidha amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa umoja na kutanguliza uadilifu na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni