Na Emanuel Madafa,Mbeya
IDADI ya vifo vya watoto wachanga imeendelea kupungua Mkoani mbeya kutoka vifo 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568 kwa mwaka 2014 ambapo ni sawa na asilimia 5.7.
Hali hiyo inatokana timu ya uendeshaji wa huduma za afya mkoa kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kuweka maazimio ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa pamoja.
Akizungumza jijini Mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani humo Ndugu Prisca Butuyuyu amesema kutokana na usimamizi huo wameweza kufuatilia mambo mbalimbali yakiwemo ya upatikanaji wa dawa .
Amesema hatua nyingine iliyofanikisha zoezi hilo ni pamoja na kushughulikia mapungufu na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika vituo vya huduma.
Amesema sanjali na mafanikio hayo pia wanatoa pongezi za dhati kwa shirika la UNICEF kwa kuendelea kusaidia kutoa fedha za usimamizi shirikishi katika eneo la huduma za afya na uzazi na mtoto.
Butuyuyu amesema kuwa baadhi ya halimashauri zimeweza kuendesha semina mbalimbali kuhusu uzazi salama ambazo ni huduma baada ya kujifungua pamoja na huduma muhimu kwa watoto wachanga.
Hata hivyo amesema shirika la UNICEF wakishirikiana na KOICA wamekuja na mpango mwingine wa miaka 4 ya uboreshaji huduma za afya ya uzazi na mtoto. Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni