Wapiga kura wa jimbo la Ohio nchini
Marekani wamekataa pendekezo la kuhalalisha uvutaji wa bangi kwa
mujibu utabiri wa vyombo vya habari.
Hatua hiyo ya uhalalishaji wa
matumizi ya bangi, inalenga kufanya mabadiliko katika Katiba ili
kuruhusu matumizi ya bangi kama tiba kwa mtu mwenye umri wa kuanzia
miaka 21.
Wapiga kampeni ya kuhalalishwa
matumizi ya bangi katika jimbo la Ohio walitumia karibu dola milioni
12, kutangaza kupigia kura uamuzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni