Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM
ambapo ajenda kuu ilikuwa kujadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa
ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu
Philipo Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia).
Kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kikiendelea ndani ya ukumbi wa
NEC, Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Muhagama muda
mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati kuu mjini Dodoma.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza
na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mhe. Zakhia Meghji muda mfupi kabla ya
kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ambayo ilikuwa na ajenda
ya kujadili majina ya wana CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea
Spika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni