KINANA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA VYAMA VYA SIASA KUSINI MWA AFRIKA MJINI MAPUTO,MSUMBIJI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Zuma Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob (kushoto) na Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Philipe Nyusi (katikati)
  Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha SWAPO cha Namibia Rais Hage Gengob, katika mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa vya Kusini mwa Afrika mjini Maputo, Msumbiji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Makatibu Wakuu wa vyama vya ANC, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU PF mjini Maputo.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Abdulrahman Kinana katikati ya wiki iliyopita aliongoza ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa Kusini Mwa Afrika.

Mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama hivyo, umemalizika mwishoni mwa wiki mjini Maputo kwa mafanikio makubwa.

Mkutano huo ulijadili masuala yaliyolenga kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya maendeleo kwa ujumla.

Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi, Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Komredi Kinana na ujumbe wake.

Ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Komredi Kinana umewajumuisha Katibu wa NEC anayeshughulikia Siasa na Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya za CCM.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni