Ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki
iliyokuwa ikitokea New York imelazimishwa kwenda Canada baada ya
tishio la bomu.
Maafisa wamesema ndege hiyo
iliyokuwa na abiria 256 ilitua salama katika uwanja wa Kimataifa wa
Halifax mashariki mwa Canada.
Polisi nchini Canada wanaendelea na
uchunguzi, hata hivyo hawakuelezea lolote juu ya tishio hilo la bomu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni