Sunday, November 15, 2015
MAKAMU WA RAIS AWAPA MOYO WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUELEKEA MCHEZO WA MARUDIANO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub
'Canavaro', baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la
dunia kati ya Taifa Stars na Algeria uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
Akizungumza
na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia,aliwataka wachezaji na
viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo,
na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano
ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
''Japo
mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na
matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo
naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo
huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,
Mtangulizeni
mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri
katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo usiku
kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote
tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa waarabu hawa wenye fitina kali
katika mchezo wa Soka''. alisema Mhe. Samia
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas
Ulimwengu, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la
dunia kati ya Taifa Stars na Algeria uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. Kulia ni Mbwana Samatta, akibugujikwa na machozi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimfariji mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, baada ya
mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa
Stars na Algeria uliochezwa
jana. Baada ya mchezo huo Samatta, alionekana kubugujikwa na machozi
muda wote. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya
Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. Picha na www.sufianimafoto.com
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishangilia sambamba na baadhi ya Viongozi bao la kwanza la Taifa Stars
lililofungwa na Elias Maguli, katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo
wa Kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia dhidi ya Algeria
uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika
mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na
Elias Maguli na Mbwana Samatta.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal
Malinzi, wakati walipokuwa Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kuwania
kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo jana
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Ila
moja kati ya kituko ilikuwa ni hiki kiti kilichokatika mguu mmoja eti
katika mchezo wa kimataifa kama huu hwakupata kiti chenye hadhi
kulingana na mchezo wenyewe
Timu zikiwa tayari kuanza mtanange huo, hapa zikipigwa nyimbo za taifa
Mudathir Yahya, akiwachora nane waarabu....
Mbwana Samatta, akitesa Waarabu kwa vyenga,akiwageuza atakavyo..
Waarabu waliimarisha ulinzi zaidi kwa Mbwana Samatta.....
Beki wa Stars, Shomari Kapombe, akiruka kwanja la mchezaji wa Algeria.....
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Algeria
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars".
Mshambuliaji
machachari wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, akionyesha umahiri
wake wa kuwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo
wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia
ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa
Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote
zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Mchezaji
wa timu ya Taifa ya Algeria, Guediora Aldane akiondoka na mpira mbele
ya beki wa Timu ya Taifa Stars, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya
kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika
mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es
salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya
kufungana Bao 2-2.
Thomas
Ulimwengu wa Taifa Stars akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu
ya Algeria, Ghoulam Faouzi, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya
kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika
mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es
salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya
kufungana Bao 2-2.
Mlinda Mlango wa timu ya Taifa ya Algeria, M'bolhi Rais akipiga shuti kuondosha mpira langoni mwake.
Mshambuliaji
wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta akiangalia namna ya kuwatoka
mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi
ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018,
katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar
es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya
kufungana Bao 2-2.
Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakishangilia ushindi wao wa awali, wakati
wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya
Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo
kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo,
Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni