Kibanda
cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John
Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA
WA MATUKIO BLOG
Askari wa
Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini,
Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza
muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais
wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam.

Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo
wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya
Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Maofisa
mbalimbali wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi
watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk
John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo

Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
Mtu
aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa
akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya
kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi
hayo.

Baadhi
ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi
ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu
aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la
heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.PICHA ZOTE NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni