SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

w1
Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
w2 
Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.
w3
Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
w5
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.
w6
Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam .Kulia nia Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma. (Picha na frank Mvungi- Maelezo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni