
Co- founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za 
duka lake la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Andrew Mahiga na rafiki ake walikuwapo.
Mbunifu wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati 
Kombe (kulia) akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo 
lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha 
Smirnoff. 
Meneja chapa (Pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) 
Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) 
Wauzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa 
kwenye banda lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi 
Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo. 
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia.
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo.
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali zitengenezwazo na wabunifu wa
 hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na 
watu mbalimbali.
Mratibu wa
 onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha Stambuli alisema 
kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa 
zao.
Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na 
vinginevyo viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza 
wigo wao kibiashara kwa kukutana na wanunuzi.
"Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na 
wanunuzi hao kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya 
mauzo wanakuwa na wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na 
kuendeleza uhusiano wa kibiashara" alisema Natasha.
Pia ametoa wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria 
maonesho mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa 
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo nchini.
Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha 
wa kufahamu aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara 
mbalimbali na kujua ni wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha 
Smirnoff inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa 
mbalimbali zitengenezwazo hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la 
kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini kuongeza pia wigo wa biashara 
zao.
Kwa upande wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya 
Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari 
(hawapo pichani) alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya 
wajasiriamali katika kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua 
kuunga mkono Pop Up Bongo.
"SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini 
Pop Up Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki 
kukutana huku wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji 
wanaouza bidhaa zao katika Pop Up Bongo" alisema Shomari.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni