Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mganga mkuu wa hospital ya mkoa wa Arusha, Dakta Frida
Mokiti, amekiambia kikao cha kamati ya maafa ya mkoa wa Arusha, kuwa hospital
hiyo inahitaji uniti 1560 za damu salama,lakini akiba ya damu salama iliyopo ni uniti 40 .
Kutokana na upungufu huo, mganga mkuu wa mkoa wa Arusha
Dakta Frida Mokiti, akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujitolea
damu nili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao matibabu yao yanahitaji damu salama.
Amesema upungufu mkubwa wa adamu unasababisha wagonjwa
wanaosubiri matibabu yanayotegemea damu salama kuwa kwenye wakati
mugumu ili kuokoa maisha yao.
Dakta Mokiti, amewaambia wajumbe wa kikao hicho cha kamati
ya maafa ya mkoa kuwa makundi makubwa yenye uhitaji mkubwa wa damu salama
kwenye matibabu yao ni wajawazito,
watoto na majeruhi .
Wajumbe wa kikao hicho ni pamoja na katibu tawala mkoa, wakuu
wa wilaya, wakurugenzi, wenye viti, madaktari wa wilaya na mkoa,sekretarieti ya
mkoa,na wataalamu wa ngazi mbalimbali na maafisa afya .
Dakta Mokiti, amesema akiba ya damu salama iliyopo ni kidogo
sana kuokoa maisha ya wagonjwa ambao matibabu yao yanahitaji damu nyingi,hivyo
anaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Dakta, Mokiti, amesema mahitaji makubwa ya damu salama yanatokana
na wingi wa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo hospital kwa ajili ya matibabu yao,na pia hospital hiyo
ya mkoa ndio inategemewa na hospital zingine kupata damu.
Kwa upande wake kaimu
katibu tawala wa mkoa huo, Anza Amen
Ndosa,aliwataka wakurugenzi wa haslmashauri za wilaya walifanyie kazi na
wasitumie bajeti kama visingizio ili kukwepa jukumu la kuchangia damu salama kupita
kwenye halmashauri zao.
Amesema uhai wa binadamu hautegeme bajeti bali damu hivyo akazitaka halmashauri kuhamasisha wananchi
kujitolea damu ili kuwezesha kupatikana akiba ya damu salama ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao matibabu
yao yanategemea damu.
Nae mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu mkoa wa Arusha,Dakta
Christopher Nzela, amekiambia kikao hicho kuwa Msalaba mwekundu,kimekuwa kikishiriki
kuhamasisha wananchi kujitolea kuchangia damu salama kwa ajili ya kuokoa maisha
ya wagonjwa wanafikishwa vhospitalini kwa matibabu .
Hamasa hiyo inayotolewa na msalaba mwekundu, imekuwa
ikisaidia kupatikana damu salama kutoka kwa wananchi wachache wanaojitokeza
kujitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa.
Nzera, amesema mwamko mdogo wa wananchi imekuwa ni
changamnoto kubwa ya kufikia malengo ya upatikanaji wa damu salama na hilo
linatokana na kuwa na uelewa mdogo na kutokujiamini kiafya.
Inawezekana wananchi walio wengi hawana uelewa wa kujitolea
kuchngia damu salama,wengine hawajiamini hivyo wanakuwa na hofu ya damu zao kukutwa
na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa
Ukimwi hivyo inakuwa vigumu kujitolea kutoa damu.
Nzera, amesema msalaba mwekundu mkoani Arusha,imekuwa ikihamasisha
vijana wa shule za sekondari na vyuo
ambao huwa wanakuwa na mwamko mkubwa wa kujitolea damu salama,wakati makundi
mengine ya kijamii yakiwa hayashiriki. MWISHO
Arusha.
SERIKALI Nimewahakikishia wananchi kuwa ulinzi na usalama
umeimarishwa kwenye kipindi chote cha siku kuu na hivyo kutoa fursa kwa
wananchi kusherehekea sikuu kuu zote bila hofu.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, ameyasema hayo jana
alipokuwa vakizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake na kuelezea hatua zinazochukuliwa
na serikali kuimarisha usalama wa wananchi na kuhakikisha kuwa usalama wa
kutosha upo.
Amevipongeza vyombo vya dola ambavyo vimekuwa vikiimarisha
ulinzi na kuwezesha wananchi wanaishi kwa usalama na amani kwa kuzuia matukio
yeyote ya uhalifu yaliyokuwa yakitishia usalama na uhai wa wananchi na mali
zao.
Kuhusu utunzaji wa mazingira, Ntibenda, amesema kuwa tayari
ameshaziagiza wilaya zote kupanga mpango kazi wa kupanda miti mwaka 2016, ili
kuondoa tatizo la uharibifu wa mazingira na ukame unaosababisha na ukosefu wa
mvua.
Amesema katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kila
mkuu wa wilaya atalazimika kufuatilia kila kaya kuhakikisha imepanda miche 30
aina mbalimbali na kuitunza ili ikue .
MWISHO.
ARUSHA.
CHAMA cha msalaba mwekundu, mkoa wa Arusha, kimekuwa
kikishiriki kikamilifu kwenye mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa kipindu pindu
ambao umedumu kwa kipindi kirefu mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Msalaba mwekundu mkoa wa Arusha, Dakta Chirstopher
Nzera, amesema kuwa Chama hicho kiliitikia wito wa serikali ya mkoa ya kuomba
wadau kusaidia mapambano ya kutokomeza ugonjwa huo.
Amesema Chama
kimekuwa kikiwatumia wanachama wake kwa kujitolea ambao wamekuwa wakishiriki mapambano hayo kwa
kushiriki kusafisha maeneo mbalimbali jijini Arusha na halmashauri ya Arusha DC.
Amesema Msalaba mwekundu,kinashiriki kwenye zoezi la
kupulizia dawa za kuuwa wadudu mbalimbali kwenye nyumba,kupulizia dawa kwenye
visima vya maji,pia kupulizia dawa kwenye vyombo vya usafiri vya abiria,na
kutembelea vituo vya biashara ambako chama kimekuwa kikitoa elimu ya kujikinga
na kuchukua hatua za maambukizi ya ugonjwa huo .
Nzera, alikuwa akitoa taarifa fupi ya utendaji kwenye kikao
cha kamati ya maafa ya mkoia wa Arusha kilichofanyika jana na kuongeza kuwa Msalaba mwekundu inakusudia
kushiriki kwenye zoezi hilo kwa wilaya zote za mkoa bwa Arusha.
Mwisho.
ARUSHA.
MAMLA ya maji safi na taka jijini Arusha,imeahidi kuboresha huduma ya maji safi kwenye maeneo
yote ambayo hayana maji ilkiwa ni hatua za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa
wa kipindu pindu.
Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA, mhandisi Ruth Koye, ametoa
ahadi hiyo jana kwenye kikao cha kamati ya maafa ya mkoa na kuahidi kuwa maeneo ambayo hayapati maji ya mtandao wa
AUWSA, na kusababisha wananchi kutumia majhi yasiyo salama watapata maji ya
AUWSA.
Amesema AUWSA, inaboresha huduma ya maji kwa awamu lengo ni
kuhakikisaha wananchi wanapata huduma hiyo ya maji safi na hivyo kuwawesha
kuepukana na ,maambukizi ya kipindu pindu kinachotokana na matumizi ya maji
yasiyo safi na salama .
Kikao hicho kiliagiza AUWSA,kuhakikisha maji yanapatikana
maeneo yote ambayo hayana maji ili kupunguza tatizo la kuenea kwa ugonjwa wa
kipindu pindu.
Aidha kikao hicho pia kimelitaka shirika la umeme nchini
Tanesco,mkoa wa Arusha, kuhakjikisha umeme kwenye vyanzo vya maji vya AUWSA,
haukatiki ili kuwezesha AUWSA, kuzalisha maji ya kutosha wakati wote .
Kikao kimesema kukatika mara kwa mara kwa umeme kwenye vituo
vya kuzalisha maji vinasababisha AUWSA, kutokusambaza maji ya kutosha na hivyo
kuwepo mgao wa maji kwa maeneo mengi ya jiji la Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni