Na manyara leo blog Arusha
SERIKALI ya mkoa wa Arusha imefuta likizo zote za watumishi
ambao walikuwa wakitarajia kwenda mapumzikoni na kuwataka waendelee na kazi kwa
kushiriki kwenye mapambano ya kutokomeza
ugonjwa wa kipindu pindu ambacho kimeendelea kuwepo mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, maarufu kijiko,
ametoa maelezo hayo alipokuwa akiahirisha kikao cha kamati ya maafa ya mko, na
kusisitiza hakuna likizo mpaka kipindu pindu kitakapotokomezwa .
Amesisitiza Kwenye hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya
ya Arusha, Fadhili Nkurlu, mkuu wa mkoa amesema hadi Desemba 23 kuna wagonjwa
14 ambao wamelazwa kwenye vituo mbalimbali na kusisitiza kuwa Arusha bila
kipindu pindu inawezekana hivyo watunishi na wananchi kwa pamoja lazima
kushirikiana ili kuondoa kabisa ugonjwa huo.
Ntibenda,amesema swala la kudhibiti ugonjwa huo linaonekana
kuachiwa idara ya afya pekee ambayo haiwezi kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa
huo hivyo sewkta zote lazima kushirikiana kuutokomeza .
Akawawaomba viongozi wa kisiasa, kijamii, kimila kushiriki kikamilifu kwenye mapambano hayo kwa kuwa ugonjwa wa kipindu pindu hauna
itikadi , hivyo akatoa wito kutolewa taarifa haraka pindi kunapotokea mgonjwa
au mwenye dalili za ugonjwa wa kipindu pindu .
Pia Ntibenda, akahimiza matumizi ya vyoo pamoja na
kuimarisha usafi wa mazingira ,sanjari na kuwachukulia hatua wale wote
watakaokuwa ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kusababisha kuendelea kuwepo
kwa ugonbjwa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni