Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
Wananchi
 wa kata ya Ngwala wilayani Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kutunza 
miundo mbinu inayojengwa katika kata yao hasa miradi ya maji ili 
waepukane na adha mbalimbali za kurudi katika adha walizokuwa wakipata 
mwanzo.
Haya
 yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akiwa Mgeni 
rasmi wakati akizindua visima viwili vilivyojengwa na kampuni ya peak 
Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya 
ardhi yanayopatikana katika kata  ya ngwala wilayanii chunya mkoani 
mbeya  ambayo hutumika kutengenezea sumaku,mota,compyuta umeme wa 
sumaku,simu ambayo kwa tanzania tanapatikana wilaya ya Chunya pekee.
Tarimo
 alisema wananchi hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa 
kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo 
hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo kwani 
mahusiona mema ndiyo chanzo cha mafanikio ya kupata maendeleo katika 
kata yao.
Akisoma
 tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo 
 meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng alisema miradi 
waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu  milioni 16kila kimoja unjezi
 wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo
 la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu  
shilingi milioni  7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.
Ochieng
 alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho 
za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali 
kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa 
kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.
Aidha
 baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja 
na Mwenyekiti wa kijiji cha  Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala 
Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na 
kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.
Maganga
 aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema 
nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza 
kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo 
unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.
Kwaupande
 wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza 
adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini
 wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio 
bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo 
awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.
Vile
 vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama 
walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji
 umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha 
shughuli nyingine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni