Nchi ya Canada imetangaza kutoa
fedha kiasi cha shilingi bilioni 2 za Kenya kusaidia wafanyabiashara
wadogo na wakati kupata mikopo ya kupanua biashara zao.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa
Canada ametoa kauli hiyo kando ya Mkutano wa Shirikisho la Biashara
Duniani (WTO), ambapo amesema fedha hizo zitasaidia kupunguza
umasikini miongoni mwa wakenya waliokwenye mikoa iliyotengwa kifedha.
Waziri huyo, Bw. Chrystia Freeland,
amesema Canada itachangia dola milioni 19.5 kwa mradi huo wa
kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wakati Kenya kwa miaka saba,
hadi mwaka 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni