Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na Meneja Masoko wa
Airtel Bi Anethy Muga kwa pamoja wakizindua promosheni mpya ya “Airtel
MKWANJIKA” itakayowawezesha wateja wote wa Airtel nchi nzima
kujishindia mamilioni ya pesa taslimu kila siku.
kikundi cha dancers kikionyesha jinsi ya kucheza wimbo maalumu wa
promosheni ya "Airtel Mkwanjika" wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo
itakayowawezesha wateja wa Airtel kushinda mamilioni ya pesa.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ijulikanayo kama “Airtel
MKWANJIKA” itakayowawezesha wateja wote wa Airtel nchi nzima
kujishindia mamilioni ya pesa taslimu kila siku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea jinsi
promosheni ya Airtel Mkwanjuka itakavyoendeshwa wakati uzinduzi wa
promosheni hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima
kujishindia mamilioni ya pesa hadi shilingi milioni 300.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifatilia uzinduzi wa wa
promosheni mpya ijulikanayo kama “Airtel MKWANJIKA” itakayowawezesha
wateja wote wa Airtel nchi nzima kujishindia mamilioni ya pesa
taslimu kila siku.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imezindua promosheni kabambe ijulikanayo kama “Airtel MKWANJIKA”
itakayowazawadia wateja wote wa Airtel nchi nzima hadi kiasi cha
shilingi milioni 300 pesa taslimu.
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga
na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa
kiwango chochote kwenye simu zao kuingia kwenye droo na kupata nafasi
ya kujishindia.
Kila siku wateja watakaoongeza salio wataingizwa kwenye droo ya
“Airtel MKWANJIKA” ambapo washindi wanne wataibuliwa na kutakiwa
kuingia katika sanduku la pesa la Airtel (Airtel Mkwanjuka Boksi) na
kujikusanyia pesa hadi kiasi cha shilingi milioni moja ndani ya dakika
moja
Akizindua promosheni hiyo,Meneja Masoko wa Airtel, Bi Anethy Muga
alisema” tumezindua promosheni hii mwisho wa mwaka ili kuwawezesha
wateja wetu kujishindia zawadi zitakazobadili maisha yao katika msimu
huu wa sikukuu. Tumeshuhudia tulivyoweza kubadili maisha ya
watanzania kupitia promosheni zetu zilizopita na leo tunaamini
promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” ni fulsa nyingine itakayoboresha
maisha ya wateja wetu wengi..”
“Airtel tunaamini wakati wa wateja wetu kutimiza ndoto zao ni sasa,
hivyo tunawahamasisha kuendelea kufurahia huduma zetu bora huku
tukiwazawadi mamilioni ya pesa kupitia “Airtel MKWANJIKA”. Huu ni
wakati wako sasa wakutumia mtandao wa Airtel kama bado hujajiunga”
alisema Muga
Akiongea kuhusu promosheni hiyo, Meneja Uhusiano, Bwn Jackson Mmbando
alisema” wateja wanaotumia mtandao wa Airtel wanaongezeka kila siku,
tunaposherehekea kwa pamoja msimu huu wa sikukuu tunamuwezesha mteja
yeyote atakaye jiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza
salio kwa kutumia vocha kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya siku
inayofata ya promosheni hii ya “Airtel MKWANJIKA”.
Mmbando alisisitiza promosheni hii ni kwa wateja wote wa Airtel,
hakuna gharama ya ziada, ili kushiriki unachotakiwa kufanya ni
kujiunga na yatosha au kuongeza salio na vocha. Tunapenda kuwajulisha
wateja wetu kuwa washindi wote watatangazwa kupitia vyombo mbalimbali
vya habari na washindi pia watapigiwa simu kutoka kwenye namba
0683-442244 kwaajili ya kuchukua zawadi zao. Hakuna tozo ya aina
yoyote mteja atakayotakiwa kulipa. Airtel inapenda kuwatahadharisha
wateja kuwa waangalifu na taarifa ambazo si sahihi wakati wote wa
promosheni.
“washindi wote watakao patikana wakati wote wa promosheni wapatiwa
kiasi cha pesa alichoweza kujikusanya na kushinda kutoka kwenye
kisanduku cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money. Droo za promosheni
hii ni za kuvutia kushiriki kwani uwezo wa mteja kukusanya pesa ndio
unaomuhakikishia kiasi cha pesa taslimu atakachojishindia” aliongeza
Mmbando.
Droo ya kwanza ya promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itafanyika tarehe
23 Desemba na nyingine nyingi zaidi kufanyika Januari 2016 na
kuendelea.
Washindi wote watapigiwa simu na wafanyakazi wa Airtel
kutoka kwenye namba 0683-442244 na kuwajulisha ushindi na siku ya
kupokea zawadi zao. Zawadi itatolewa kwa mteja ambaye jina lake
litafanana na usajii wa namba yake pamoja na kitambulisho chake
Masanduku ya pesa yatawekwa katika maeneo ya miji mikubwa
na washindi walioko maeneo hayo watatakiwa kuja mjini ili kuzungusha
sanduku na kukusanya pesa za ushindi
Washindi wote watatakiwa kuchukua zawadi zao kabla ya tarehe
30 Machi 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni