MADEREVA WAHIMIZWA KUTOTUMIA KILEVI WANAPOENDESHA MAGARI

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SGT. Tunu Kuta(kulia) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Masoud Seleman ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo hicho katikati Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa huo SSP Nuru Selemani na wapili kulia ni Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani.
Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)akimpa maelezo dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud Selemani kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Dodoma.Katikati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani.
Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa elimu kwa abiria ndani ya basi liliendalo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Dodoma ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani(kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)Kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.Wengine kutoka kusho ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa kampuni hiyo Heladius Kisiwani.
Baadhi ya Madereva wa mabasi yanayosafirisha abiria mikoani wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia) akiwapatia elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Shughuli ikiendelea ya kutoa elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.

Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani,leo imefanyika katika Mkoa wa Dodoma.

Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani  amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa Dodoma  ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani  kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua hususani katika kipindi hiki cha msimu unakoelekea wa sikukuu na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Kwa upande wake,Kaimu  Mkuu wa kanda ya kati wa asoko wa Vodacom Tanzania Heladius Kisiwani, alisema Vodacom itaendelea  kushirikiana na serikali katika kuunga mkono jitihada za kuondoa  matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia sheria za barabarani na kutokutumia simu wakati wowote wakiwa wanatumia vyombo vya moto".

 Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu  ya mkononi  kupitia kampeni  ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

 Alisema kampuni hiyo itaendeleza kutoa elimu kwa mikoa mingine pia katika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Morogoro,Dar es Salaam na mikoa mingine na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa  usalama barabarani  walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendesha vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Dodoma wamesema ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Sunday Israel mkazi wa Dodoma aliyekuwa safarini kuelekea Singida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni