Mshindi wa tuzo ya Nobel Malala
Yousafzai amemlaumu mtia nia ya urais wa Marekani kwa tiketi ya chama
cha Republican, Donald Trump, kwa kauli yake ya kutaka waislamu
wasiruhusiwe kuingia Marekani.
Malala ambaye alipigwa risasi ya
kichwa na Wataliban kwa kutetea elimu ya mtoto wa kike, amesema
matamshi hayo ya Trump yalijaa chuki, na kuwashutumu waislam wote kwa
ugaidi, kutachochea idadi ya waislam wanaojiunga na ugaidi.
Malala alikuwa akiongea katika tukio
la maadhimisho tangu kufanyika shambulizi la wapiganaji wa Taliban
katika shule moja huko, Peshawar, Pakistan na kusababisha vifo vya
watu zaidi ya 140, wengi wao wakiwa watoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni