Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kumkamata
mtuhumiwa wa mauaji ya mfanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa,na mkuu wa
Taarifa Fiche wa shirika hilo Emily Kisamo aliyeuwawa mwishoni mwa wiki katika eneo la Kikwakwaru Kata ya
Themi jijini Arusha.
Akizungumza
na vyombo vya habari ofisini kwa kwake jijini hapa Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani hapa Liberatus Sabas alisema jeshi hilo limefanikwa kumkamata mtu
anayeitwa Ismail Swalehe Sang’wa 20 mtunza bustani mkazi wa Sepuka Wilayani
Ikungi mkoani Singida.
Alisema kuwa
siku ya tukio mtuhumiwa alimvizia marehemu akinywa uji Sebuleni na kumkata
shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali,baada ya kukamatwa mtuhumiwa aliweza
kueleza jinsi alivyotekeleza mauaji hayo huku akieleza pia sababu za kufanya
hivyo ni tama ya pesa alizokuwa nazo marehemu hapo kiasi cha tsh. Million 5.
Kamnda Sabas
aliendelea kusema kuwa baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa alikiri kwamba
alianza usafi wa ndani ya nyumba kwa kupiga deki na kasha kulisafisha gari kwa
nje na kuliendesha mpaka eneo alipolitelekeza gari la marehemu Kisamo.
Mara baada
ya upekuzi polisi waligundua vitu kadhaa kwenye gari hilo vikiwemo fedha
taslimu kiasi cha Tsh.Milion 4.29,4000,simu za mkononi tatu. Aina ya Samsung,na
vocha aina ya Vodacom za 5000 zenye thamani ya 70000 vyote hivyo vilifukiwa
kwenye banda la kuku.
Pia polisi
waligundua panga moja lililokuwa na damu ambalo lilikutwa stoo na vitu vingine
kama taulo kubwa nne,kitambaa cha mezani,suruali moja ya mtuhumiwa ambazo
zilifichwa kwenye migomba karibu na mabanda ya kuku na zilikuwa na damu ambapo
ndizo zilitumika na myuhumiwa kupigia deki ndani baada ya kumuua marehemu.
Kamanda
alisema kuwa kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na
upelelezi na pindi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Wakati huo
huo jeshi la polisi liemsema kuwa limejipanga kuhakikisha wakazi wa mkoa huo
wanasherehekea sikukuu zote Maulid na Krismas kwa amani na utulivu na kuwataka
wakazi wote kuhakikisha hawafanyi vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa
amani.
Kamanda wa
jeshi Hilo mkoani hapa Liberatus Sabas pia akawatakiwa wakazi hao sikukuu njema
na yenye Baraka itakayoendana na kukukaribisha mwaka bila ya kuvunja sheria za
nchi na kufanya matukio ya fujo na kushrehekea kwa amani sikukuu hiyo
Mwisho……………………………………………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni