SERIKALI WILAYANI CHUNYA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WAJIPANGA KUTATUA KERO ZA MAJI WILAYANI HUMO

Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 

                                                                Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya,Jamiimojablog
 

Serikali WIlayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa maji wilayani humo.


Hatua hiyo inakuja kufuataia kampuni ya Peak Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi yanayopatikana katika kata ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya shilingi milioni 16.


Akizungumza wakati wa makabidhiano ya visima hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Elias Tarimo amesema hatua ya kampuni huyo inayojihusisha na utafiti wa madini kuamua kuchimba visima hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ni jambo jema nalinalotakiwa kuungwa mkono na wananchi hao.
 

Amesema katika kuunga mkono jitihada hizo wananchi hao hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo.

 

Akisoma tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng amesema miradi waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu milioni 16kila kimoja unjezi wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu shilingi milioni 7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.


Ochieng alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.


Aidha baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.
 

Maganga aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.
 

Kwaupande wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.
 

Vile vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha shughuli nyingine.
Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni