Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha
Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya
(kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya
4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha
Kazaura (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu
ya uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE inayotolewa na kampuni hiyo. Kushoto
ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akiwa
katika mkutano huo.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota (kushoto)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla
ya TTCL kuzinduwa teknolojia ya 4G LTE iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania
(TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha
Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya
(kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya
4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE toka TTCL leo.
Kulia
ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa
ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya
uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE.
Kulia
ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa
ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya
uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE.
Kushoto
ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL na maofisa
waandamizi wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki
katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE.
KAMPUNI
ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imezinduwa mtandao unaotumia
teknolojia ya 4G LTE unaoanza kutoa huduma jijini Dar es Salaam. Mtandao
huo wenye teknolojia mpya na ya kisasa wenye kasi kubwa utatoa huduma
katika maeneo 11 ambayo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K.
Nyerere, Pugu Road, Posta Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay,
Mwenge, Mbezi Tangibovu, Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala, na Wazi
Tegeta.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam wakati akizinduwa rasmi teknolojia hiyo, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema licha ya kuzinduwa
huduma hiyo katika maeneo 11 kwa sasa mafundi wa kampuni hiyo wapo
kazini wakiendelea na awamu ya pili ya kufunga mitambo ili huduma hiyo
itolewe pia katika maeneo mengine 14 ya jiji la Dar es Salaam.
Aliyataja maeneo mengine ambayo mitambo inaendelea kufungwa kwa sasa
kuwa ni pamoja na Kigamboni, Masaki, Temeke, Kimara, Jangwani, Kariakoo,
Chuo Kikuu, Kurasini, Mbezi Chini Gongo la Mboto, Tabata, Kibamba,
Kongowe na Bunju.
"...Awamu ya pili ya mradi huu itakuwa imekamilisha maeneo yaliyobaki
ya mkoa wa Dar es Salaam na pia kupeleka mawasiliano hayo katika mikoa
mingine ikiwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko,"
alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura.
Alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE unakuwa umekamilisha nia ya
siku nyingi ya kampuni ya TTCL ya kuwahudumia wateja katika nyanja zote
za mawasiliano (Fixed-mobile convergence) kwa kutumia teknolojia ya simu
za mezani na simu za mkononi.
Akifafanua zaidi Dk. Kazaura alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE
utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuongeza kasi ya shughuli za
maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuchangia katika kukuza teknolojia ya
habari na mawasiliano na pia kuongeza uzalishaji kwenye sekta
mbalimbali za maendeleo.
Aidha aliongeza kuwa TTCL inaamini mtandao wa 4G LTE utafungua fursa
pekee katika kukuza sekta ya elimu nchini kwa njia ya mtandao (E
education). Na pia ubora wa huduma hiyo ya intaneti utatoa fursa kwa
wanafunzi, wakufunzi, wataalam, wanazuoni na walimu kutumia teknolojia
katika kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na nje ya taaluma.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL,
Peter Ngota akifafanua zaidi kwa wanahabari alisema mtandao wa 4G LTE
utaongeza fursa katika sekta ya afya ambapo hospitali, vituo vya afya,
vyuo vya afya na wadau mbalimbali wataweza kutumia mtandao huo katika
kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi tena kwa
haraka zaidi.
Alisema
mtandao huo pia utazinufaisha sekta nyingine za kiuchumi kama vile
sekta ya biashara, viwanda, kilimo na nyinginezo. "...Wafanyabiashara na
wazalishaji wa bidhaa wanahitaji mawasiliano ya uhakika katika shughuli
zao. Mtandao huu wa 4G LTE utakuwa mkombozi wao na utaleta mageuzi
katika kuongeza uzalishaji, kupanua wigo wa masoko ya bidhaa kwa
wakulima, masoko kwa wajasiliamali, masoko kwa makampuni ndani na nje ya
mipaka ya Tanzania," alisema Peter Ngota.
Hata hivyo, Ngota aliongeza kuwa uzinduzi huo unaenda sambamba na
uboreshaji vifurushi rafiki vya intaneti kwa wananchi hivyo kuwaomba
wananchi kuiunga mkono kampuni ya kizalendo ya TTCL katika kuboresha
huduma za mawasiliano nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni