SHIRIKA LA UJASUSI LA FBI LASEMA WANANDOA WALIPANGA NJAMA ZA KIGAIDI KABLA YA KUOANA

Shirika la Ujasusi la Marekani FBI limesema wanandoa waliofanya tukio la shambulizi la San Bernardino na kuuwa watu 14 walingizwa katika itikadi kali kabla ya kuanza mahusiano yao.

Bw. James Comey amesema Tashfeen Malik na mumewe Syed Farook walizungumzia masuala ya Jihad katika mazungumzo yao kwenye mtandao wa kutafuta wenza mwaka 2013.


Shirika la FBI linaamini wanandoa hao walifanya tukio hilo kutokana na kuvutiwa na matukio ya makundi ya kigaidi, hata hivyo uchunguzi unaendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni