Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiangalia Sehemu ya
mtaro wa maji katika eneo la Tegeta, Basihaya wilayani Kinondoni, Jijini
Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo
ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo,
kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mkazi wa
Tegeta, Basihaya Jijini Dar es Salaam, Jumanne Malongo alipokuwa
akimueleza jinsi wembamba wa mtaro huo unavyosababisha maji kujaa katika
makazi yao, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo
ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo,
kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Manisipaa kinondoni, Ando Mwakunga akimueleza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), uharibifu wa
“kalvati” katika eneo la Boko, Ununio Jijini Dar es Salaam, leo wakati
Waziri huyo alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa
kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiteta na Mkurugenzi
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya juu
ya ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani, Buguruni wilayani
Ilala, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi
wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha
jijini humo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akitoa maelekezo baada
ya kutoridhishwa na ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani,
Buguruni Ilala Jijini Dar es Salaam, kwa Uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa hiyo kumpatia taarifa ndani ya siku tano inayoeleza ni jinsi
gani watakavyokamilisha ujenzi huo, leo wakati alipofanya ziara
kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua
zinazoendelea kunyesha jijini humo.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni