Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Azaaza Kutekeleza Ahadi Zake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kwa Ujenzi wa Ukuta Kituo cha Afya Chumbuni

Katibu wa UVCCM Jimbo la Chumbuni Saadam Saleh akitowa maelezo wakati wa Mkutano wao na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa katika ziara yake kuwatembelea Vijana wa UV CCM Zanzibar
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Amani Unguja Ali Seif akizungumza na Vijana wa Jimbo la Chumbuni wakati wa ziara ya Katibu wa UVCCM Mhe Shaka Hamdu Shaka akiwa katika ziara yake kutembelea Vijana Zanzibar.
Afisa wa UVCCM kutoka Makao Makuu Dar-es-Salaam Fatma Rashid akizungumza na Vijana wa UVCCM wa Jimbo la Muembemakumbi Zanzibar wakati wa ziara yao kutembelea Vijana Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mhe Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kutoa nasaha zake kwa Vijana wa CCM wa Jimbo la Muembemakumbi wakati waziara yake kutembelea Jumuiya za Vijana Zanzibar. mkutano huo umefanyika katika Afisi za Tawi la CCM Chumbunin Karakana.
Vijana wa CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa UVCCM wakati wa mkutano wake na Vijana hao Tawi la CCM Chumbuni Karakana
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar na Kamanda wa Vijana Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Vijana wa UVCCM Tawi la Chumbuni wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Vijana Mhe Shaka Hamdu Shaka kutembelea Jumuiya za Vijama katika Majimbo ya Zanzibar.
Vijana wa CCM wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa mkutano ziara ya Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Mhe Shaka Hamdu Shaka,mkutanom huo wa Vijana umefanyika tawi la CCM Chumbuni Karakana
Mbunge wa Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa na Katibu Mkuu wa Vijana CCM TanZania Mhe Shaka Hamdu Shaka wakielekea katika ujenzi wa Taifa wa kuchimba msingi wa ukuta wa Kituo cha Afya cha Chumbuni ikiwa ni moja ya ahadi za Mbunge kukiimarisha Kituo hicho kwa kuaza ujenzi wa Ukuta ikiwa nin hatua za mwazo za kukiimarishas kituo hicho kutoa huduma bora kwa wananchi wa jimbo la chumbuni na jirani zao.
Mhe Mbunge AMJAD akichimba msingi wa ujenzi wa ukuta wa kituo hicho cha Afya Chumbuni Zanzibar.
Mbunge AMJAD na Katibu Mkuu wa Vijana Mhe Shaka Hamdu wakichimba msingi wa ujenzi wa kituo cha afya chumbuni Zanzibar. 
Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Pondeza AMJAD akishgiriki katika ujenzi wa taifa wa uchimbaji wa msingi wa kituo cha Afya Chumbuni ikiwa ni ahadi yake ya kujenga ukuta huo kukiweka katika mazingira mazuri kituo hicho cha Afya Chumbuni kwa ajili ya kutowa huduma bora. 
Vijana wa CCM Jimbo la Chumbuni wakiwa katika ujenzi wa Taifa wa Kituo cha Afya Chumbuni Zanzibar ikiwa ni moja yac ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo kwa wananchi wake kukiimarisha Kituo hicho cha Afya.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar akitimiza ahadi kwa Wananchi wake kwa kujenga Ukuta kwa ajili ya Kituo hicho kwa hatua ya mwanzo ya kukiimarisha kituo hicho kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya kwa masaa 24.  Imetayarishwa na zanzinews.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni