Gari
la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.
Ummy Mwalimu likiwasili Makao Makuu ya wizara hiyo na kupokelewa kwa
saluti mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika leo Ikulu
jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando mara tu
baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia)
kuelekea ofisini kwake.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake huku Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Dkt. Donan Mmbando akishuhudia tukio hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akiwasili katika wizara ya hiyo moja kwa moja akitokea Ikulu
baada ya kula kiapo.
Pichani
juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi
wa wizara hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akimkaribisha Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwake.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) akisalimiana na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akitoa taarifa ya maendeleo ya
Wizara kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon
Malabeja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni