Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini
katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo
Jumamosi.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-
Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella
Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake
baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia)
akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara
baada kufika ofisini kwake kuanza kazi leo Jumamosi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (wa pili kutoka
kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji wa ofisi yake mara
baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi
na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.
…………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
(MB) ameanza kazi rasmi Leo Jumamosi Desemba 12/2015 mara baada ya
kuapishwa Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
Mhe. Kairuki akiongea na watendaji
wa Wizara yake alielekeza masuala ya kiutumishi ikiwamo kusimamia
nidhamu ya kazi ni jambo la msingi hivyo kutumia daftari la mahudhurio
peke yake haitoshi.
“Tutumie Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) ili kubaini Watumishi wanaoiba muda wa kazi wa
Serikali” Mhe. Kairuki alisisitiza na kusema kazi lazima zitekelezwe
kwa kiwango cha juu.
Mhe. Waziri Kairuki alisema suala
la kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ni
muhimu kwa kuwaelekeza watendaji wa Wizara yake kushirikiana na Wakala
ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kubaini taarifa za watumishi
wanaofariki ili wafutwe katika orodha ya malipo.
Mhe. Waziri Kairuki alisema
ushirikiano katika kazi ni jambo la msingi ili kushauriana katika
kutatua changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala
mbalimbali ya kiutumishi na kuondoa malalamiko.
Awali, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda akimkaribisha Mh. Waziri
Kairuki kuongea na watendaji wa Wizara alisema waajiri wote nchini
walishaelekezwa kufanya kazi ya kusafisha takwimu zisizohitaji katika
Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini
(HCMIS).
Bw. Nzunda alisema Watumishi wote
wenye takwimu chafu (takwimu zisizohitajika) katika mfumo wa HCMIS
watafutwa baada ya kukamilika kwa zoezi hilo ifikapo mwisho wa mwezi
Desemba 2015 na endapo kutakua na mwajiri atakayekua na takwimu chafu
atawajibika kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni