Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza 
wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na 
Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la 
linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). 
Na Rabi Hume.
Mratibu
 wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez 
amezitaka serikali za nchi za Afrika ikiwemo serikali ya Tanzania 
kutekeleza vyema sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuhuisha sera
 ya viwanda kwa ajili ya mipango ya ukuzaji wa viwanda.
Kauli
 hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu 
Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa 
la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). Shughuli 
iliyofanyika Chuo cha Diplomasia cha Msumbiji na Tanzania, kilichopo 
Kurasini Dar es salaam.
Katika
 hotuba yake hiyo alisema suala la Sera za ubunifu ni mpya kwa mataifa 
mengi ya Kiafrika na hivyo hazitekelezwi vyema na kusema pia mifumo ya 
uvumbuzi inakabiliwa na changamoto nyingi.
Alisema sera nyingi za viwanda katika nchi za Afrika hazikujenga mfumo wenye kuchagia mafunzo ya teknolojia na utekelezaji wake.
Naibu
 Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Bw. 
Bernard Achiula akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa kabla ya 
kumkaribisha Mratibu Mkazi wa UN nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (hayupo 
pichani).
“Na
 hata kama kuna sera za maendeleo ya viwanda sera hiyo haikuratibiwa 
vizuri na suala la sayansi teknolojia na uvumbuzi.” Alisema.
Alisema
 wakati umefika kwa nchi za Afrika kuhakikisha kwamba zinaoanisha yote 
hayo ilikuwa na sera madhubuti ya mazingira yenye lengo la kuendeleza 
viwanda, teknolojia na sayansi vikiwa pamoja.
Hafla
 hiyo imefanyika ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Mataifa (UN) kuzindua
 ripoti inayohusu Teknolojia na Ubunifu duniani 2015 jijini Geneva, 
Switzerland, ofisi ya UN Tanzania imezindua ripoti hiyo nchini na 
kuonyesha hali iliyopo Afrika.
Dkt.
 Bitrina Diyamett kutoea Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, 
Teknolojia na Ubunifu (STIPRO), akidadavua ripoti ya mwaka 2015 
inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa
 Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kabla ya 
kuzinduliwa rasmi kwa ripoti hiyo.
Akizungumzia
 uzinduzi huo, mdadavuzi wa ripoti hiyo, Dkt. Bitrina Diyamett kutokea 
Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STIPRO) 
alisema katika taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Shirika la Umoja wa 
Mataifa linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonyesha 
jinsi ambavyo Tanzania na nchi nyingine za kiafrika zisivyokuwa na sera 
nzuri za viwanda na ubunifu.
Alisema
 katika tafiti ambayo imeanza kufanyika mwaka 2000 katika nchi zaidi ya 
10 za Afrika kunaonekana serikali za Afrika zinashindwa kutofautisha 
sera viwanda na sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na hivyo 
kushindwa kukuza viwanda na kuwasaidia wazalishaji wa nchini sababu sera
 hizo ndiyo zinazowaunganisha.
Katika
 utafiti huo uliofanywa na UNCTAD unaonyesha kuwa mauzo ya bidhaa 
zinazotengenezwa kwa teknolojia ya juu umefikia asilimia 52 mpaka 2014 
na umekua kwa asilimia 18 duniani kote kuanzia mwaka 2000 na Afrika 
umekua kwa asilimia 0.3 kati ya asilimia 18 ambazo zinaonekana kukua 
tangu 2000.
 
Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) 
akiongozana na Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chu cha 
Diplomasia, Bw. Bernard Achiula (suti nyeusi) mara baada ya kuwasili 
wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa Mozambique uliopo katika Chuo 
cha Diplomasia jijini Dar es Salaam.(Picha na Modewjiblog).
Aliongeza
 kuwa ili sera hizo zifanye kazi zinahitaji kushirikiana lakini kwa 
Afrika hakuna ushirikiano na kuwa katika wakati mgumu ya kuzifanyia kazi
 sera hizo.
"Wamefanya
 utafiti lakini Afrika hali sio nzuri shida zilizopo hakuna ushirikiano 
kila mtu anakuwa kivyake, hawa wanafanya kazi kwa kuangalia sera yao 
kivyao na hawa wanafanya kivyao kwahiyo kufanikiwa inakuwa shida,
"
 Ukiangalia kwa Afrika hata katika nchi ambazo zinajitahidi kwa sera 
hizo kuwa sehemu moja lakini watekelezaji wake hawana umoja kwamba wakae
 pamoja kuona jinsi wanafanya sasa unakuwa kama ugomvi kila mtu kuona ni
 sera yake na hakuna kitu kinafanyika," alisema Dkt. Bitrina.
Dkt.
 Bitrina alisema kutokuwepo kwa ushirikiano kunafanya kupotea kwa fedha 
nyingi kwa sababu serikali inakuwa inatoa pesa nyingi kutekeleza sera 
moja na ikitoa tena pesa nyingine kwa utekelezaji wa sera nyingine 
lakini kama sera hizo zikifanya kazi kwa kushirikiana kuna uwezekano wa 
kuokoa pesa hizo.
Aidha
 alitoa ushauri kwa serikali kupitia upya sera ya viwanda na sera ya 
sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuzifanya sera hizo kufanya kazi kwa 
pamoja na kuweza kuinua viwanda ambavyo ndiyo vinatoa ajira nyingi na 
kama watafanya hivyo wataweza kupambana na ukosefu wa ajira nchini na 
kuokoa pesa nyingi.
Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizundua rasmi 
ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa 
na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na 
Maendeleo (UNCTAD). Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na 
Fedha wa Chu cha Diplomasia, Bw. Bernard Achiula na kushoto ni Dkt. 
Bitrina Diyamett kutoea Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, 
Teknolojia na Ubunifu (STIPRO).
Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, Dkt. Bitrina 
Diyamett na Bw. Bernard Achiula kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa 
wageni waalikwa na wanahabari.
Mshehereshaji
 Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Stella Vuzo, 
akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa kipindi cha maswali na 
majibu kwenye uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na 
Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la 
linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). 
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wakiwemo wakufunzi na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiuliza maswali meza kuu.
Pichani
 juu na chini ni wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia na wakufunzi wa chuo 
hicho waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu 
Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa 
la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni