SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAUNGANA NA COGNIZANT KUBORESHA HUDUMA KWA WAGENI WAKE DUNIANI.

SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu na Cognizant (NSADAQ: CTSH), shirika linaloongoza kwa huduma za teknolojia ya habari, ushauri na biashara, leo wametangaza makubaliano ya kimkakati yatakayoendesha mabadiliko ya kidijitali pande zote za shirika hilo pamoja na washirika wake.



Chini ya mpango wao wa miaka mitatu wenye thamani ya mamilioni ya madola, Cognizant watawasaidia Etihad kufafanua mkakati wao wakidigitali na kutengeza dhana mpya ambayo itatumika katika kutoa huduma bora kwa wageni wao watakaosafiri popote na ndege za Etihad.

Kwa kuleta pamoja mikakati ya kidijitali, teknolojia, sekta na uzoefu wa ubunifu, Cognizant watafanya utafiti wa hali ya sasa ya biashara na teknolojia ya shirika la ndege la Etihad na kutumia utafiti huo kutengeneza mazingira ya kidijitali ya kiwango cha hali ya juu, itakachowezesha usambazaji kupitia idhaa nyingi, ugawaji wa wateja kwa kina zaidi na kubinafsisha ujuzi katika masoko.

Kwa kutumia taarifa mbalimbali na ufahamu wa mteja, Cognizant italiwezesha shirika la ndege la Etihad na washirika wake, kuelewa zaidi mahitaji ya wageni wake.

Kwa kuunganisha tafiti hizi na mazoea bora, michakato na teknolojia, shirika hilo litawapa wageni wake suluhisho, ofa zitakazoendana na kila mteja kwa mapenzi yake na itaboresha huduma zinazotolewa katika safari nzima kutokana na hali ya uaminifu wao na upendeleo wa mteja kama vile bidhaa na huduma, kuchagua wapendapo kukaa wakati wa safari, chaguo la mlo, safari kipindi cha sikukuu na kadhalika. Kwa shirika hili, hii inamaanisha kufungua mitiririko mipya ya mapato, kuongeza chapa na kutengeneza fursa nyingine za kibiashara.

Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika la Etihad Peter Baumgartner, alisema, “Wageni wetu wamezidi kugeukia idhaa za kidijitali zaidi kujiunga nasi na hivyo tunatambua umuhimu wa kuwafikishia ubora wa kipekee na usio wa dosari katika sehemu zote tunazofikia. 

Ushirikiano wetu na Cognizant utatusaidia kufikia kiwango bora katika safari za kidijitali ambayo itawaburudisha wateja kuanzia kupanga safari hadi kununua tiketi, kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege, na itaboresha uaminifu wa wageni kwa kuwavutia na kuwashirikisha wageni katika njia mpya na za kisasa.”

Robert Webb ambae ni Afisa Mkuu Habari na Teknolojia wa shirika la Ndege la Etihad, alisema “Ushirikiano huu ni muhimu kwa mikakati yetu teknolojia na uvumbuzi ambayo hutuimarisha na washirika wetu katika kujipanga upya kuwapatia wageni wetu huduma bora katika safari zao ambayo inaendana wakati wa safari na tamati yake. 

Tumechagua Cognizant kwa sababu wanaongoza katika programu za kidijitali, uzoefu wa kidigitali kwenye huduma za usafiri, ukarimu na ushirikiano wa muda mrefu na shirika na pia ni viongozi katika dunia ya teknolojia.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa Cognizant, Francisco D’Souza, alisema: “Tumefurahia kushirikiana na Etihad kutengeneza shirika la ndege lenye kuwapa kilicho bora wateja wake wakati wa safari zao kwa kutumia nguvu ya teknolojia ya kisasa. Kwa Cognizant, mfumo wa kidijitali’ inamaanisha kuwa na uwezo wa kuunganisha teknolojia, takwimu za kisayansi, vifaa, ubunifu na mikakati ya kibiashara kubadili mifumo na uzoefu.

 Ushiriki huu unaweka alama ya kuungana kwa mashirika mawili yenye kasi ya uongozi ambayo mikakati yao ya ukuaji inabebwa na uvumbuzi wa kidijitali. Timu ya kazi za kidijitali ya Cognizant inafurahia na kutegemea mengi kwa kusaidiana na shirika la ndege la Etihad pamoja na washirika wake ikiwemo kuleta udhibiti, urahisi na uwazi kwa msafiri wa kisasa. 

Muamko wa kidijitali utazidi kuimarisha shirika la Etihad katika kuwa na chapa yenye kiwango cha hali ya juu kwa kutoa huduma bora kwa wateja.




Kama sehemu ya ushirikiano huu, Cognizant itasimamia program za Etihad na kuziunganisha katika jukwaa jipya la kidijitali. Kituo cha ubora wa kidijitali itaanzishwa kuendesha uvumbuzi pamoja na washirika wakuu wa kiteknolojia wa Etihad.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni