Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa
(katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
alipotembelea eneo la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda
ya kusini, mkoani Mtwara.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimuuliza swali Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Ligula ya mkoa wa Mtwara Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) wakiwa eneo
la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini, mkoani
Mtwara.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (kushoto)
inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini inayojengwa eneo la
Mikindani mkoani Mtwara.
Muonekano
wa moja ya majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini
itakayohudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma inayojengwa eneo la
Mikindani mkoani Mtwara.(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO).
Na Mwandishi wetu, Mtwara
UJENZI wa hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini, unaofanyika mkoani Mtwara sasa upo katika majengo ya wagonjwa wa nje (OPD).
Ujenzi
huo ulioanza mwaka 2009 kwa kusafishwa kwa eneo na kujengwa kwa uzio wa
kilomita 2.7 mwaka 2011 kwa gharama ya shilingi milioni 840 na kuanza
kujengwa kwa majengo ya OPD mwaka 2013 umelenga kuwezesha mikoa ya
Kusini kuwa na hospitali kubwa yenye hadhi ya kisasa.
Akisoma
taarifa ya maendeleo ya ujenzi kwa Naibu Waziri katika wWizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla,
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara alisema kwamba ujenzi wa mapokezi
umetarajiwa kutumia shbilioni 4.8 na hadi sasa wametumia bilioni 1.8
Mganga huyo alisema mradi mzima unatarajiwa kujengwa kwa bilioni 78.
Alisema
kuchelewa kuendelea japo sasa wana ghorofa 2 zilizoezekwa na wanapiga
ripu kunatokana na upatikanaji wa fedha kutoka serikali kuu.
Alisema
hospitali hiyo ni muhimu sana kukamilika kutokana na kukua kwa uchumi
wa Mtwara na mikoa jirani na pia kuwapo kwa uhitaji kwa mikoa ya
kaskazini mwa nchi jirani.
Naye
Naibu Waziri Kigwangwalla alisema kwamba ni matumaini yake kuwa
hospitali hiyo itakamilika mapema na kubakiza changamoto za matumizi ya
wananchi kutoka nchi jirani ambao kwa sasa wanafaidika sana na hospitali
ya Ligula.
Alisema
wataalamu wanatakiwa kuangalia hali hiyo ili kuwepo na matumizi sahihi
ya miundombinu hiyo iliyolenga kufaidisha wananchi wa Tanzania.
Aidha akiwa Mtwara Naibu Waziri huyo aliendelea kusisitiza watumishi wote kuwajibika na kuwahi maeneo yao ya kazi.
Alisema
watumishi wa umma wanaofikia laki nne wamepata nafasi adimu ya
kuutumikia umma wa watu takribani milioni 50 na hivyo ni lazima
waheshimu watanzania kwa kuwatumikia ipasavyo.
Alisema
wao waliomba nafasi ya kuhudumia watanzania kwa hiyo ni lazima
wawahudumie watanzania na kila mmoja katika kitengo chake ni lazima
kuhakikisha watumishi wanafanya kile walichoahidi katika mikataba yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni