Wazazi wa marehemu Doto Mzava wakitoa heshima za mwisho kwa mtoto wao mpendwa. |
Baadhi ya wanandugu na marafiki wakitoa heshima za mwisho . |
Baadhi ya marafiki ,ndugu na majirani waliotoka maeneo mbalimbali kushiriki maziko ya marehemu Doto |
Jeneza lenye mwili wa marehemu Doto likitolewa ndani ya nyumba . |
Mmoja wa wakurugenzi wa Jamii Media group Maxence Melo alikua miongoni mwa waombolezaji katika mazishi ya mmoja wa wafanyakazi wake wa mtandao wa Jamii Forum. |
Hali ya Majonzi ilitawala nyumbani hapo |
Mchungaji wa kanisa la Adventista Wasabato ,Mchungaji Ezekiel akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Doto. |
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Doto tayari kwa ajili ya kuwekwa kwenye nyumba yake ya milele. |
Jeneza likishushwa kaburini. |
Mchungaji Ezekiel akisoma neno mbele ya kaburi. |
Mchungaji akiweka mchanga kaburini. |
zoezi la kufukia kaburi likaanza . |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika maziko ya marehemu Doto kijijini Vudee wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. |
Mmoja wa Wanachama wa kundi la Mtandao la MADA MOTO la mjini Moshi ,Charles Ndagula akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kundi hilo ambalo Doto alikuwa mwanachama wake. |
Kiongozi wa kundi la Prince Media akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama wa kundi hilo ambao walisoma na marehemu Doto. |
Mweka hazina wa Arusha Press Club (APC) Pamela Mollel akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanahabari wa mkoani Arusha |
Salamu za Rambi rambi zilitoka maeneo mbalimbali. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni