Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo.
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati alipofanya ziara katika Daraja la Kigamboni.
Sehemu ya Daraja la Kigamboni.
Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja
wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo
akimuonesha Waziri muunganiko wa barabara zinazoingia katika daraja
hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Waziri Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau
akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhusu
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati waziri huyo
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo
ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk.
Ramadhani Dau (katikati) wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo
ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni
Meneja Mradi ujenzi wa Daraja hilo. Mhandisi Kareem Mataka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia), alipofanya
ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo ujenzi wake
utakamilika Januari Mwakani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati
alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo
ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), kuhakikisha linakabidhi daraja la Kigamboni ifikapo Januari, 2016.
Pia ametoa fursa kwa shirika hilo na mengine nchini
kama yataweza kuja na mradi wa ujenzi wa daraja kutoka Dar es Salaam hadi
Zanzibar.
Hayo alibainisha jana jijini Dar es Salaam wakati
alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo, ambalo linatarajiwa
kukamilika mwakani.
Alisema ujenzi wa daraja hilo, umegharimu kiasi cha
Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa
asilimia 60 ya fedha zote.
“Tunaliomba shirika hili, lihakikishe linaheshimu nha
kuzingatia muda uliotoa katika kukabidhi daraja hilo mwakani licha ya
kujitokeza ujenzi mwingine wa barabara ya Kilomita moja,”alisema.
Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja
ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha
ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.
Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi
ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia
Seriali katika kukuza uchumi.
“Miradi ya namna itasaisdia kukuza uchumi wa ndani na
nje ya nchi, pia inatufundisha kujifunza ili kujua kwamba tunaweza kuhimili
miradi mingine mikubwa zaidi ya huu,”alisema.
Kuhusu daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar,
alisema uwezekano wa kujengwa upo endapo mashirika yakijitokeza na mradi huo. “Kila kitu kinawezekana, hivyo kama Shirika
litajitokeza serikali ipo tayari kwa kila kitu kuunga mkono mkakati watakao
kuja nao,”alisema.
Naye Mkurungenzi wa NNSF, Dk.Ramadhan Dau alisema ujenzi
wa daraja hilo umekuwa wa kasi licha ya matatizo yaliyojitokeza, hivyo
Watanzania watarajie Januari mwakani
kulitumia.
“Bado kuna sehemu nyingine ambazo tutamalizia ila
hadi Januari litakuwa limekamilika kwa asilimia 100, hivyo tunaipongeza serikali
kwa ushirikiano uliotuonyesha,”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni