Baadhi
ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na
waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea
matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao
kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao.
Mdau Krantz
Mwantepele akihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano (Aliyejishika tama )
ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya
mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi
katika kijiji hicho.
Picha
ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani na
waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na
kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji
hicho.
Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA
Mkutano
mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga
uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi
wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule Azimio hilo Pia limeelekezwa
kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli
mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika
mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji Iikihusisha
mapato na matumizi.
Mkutano
huo umepitisha maazimio matano yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima
kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji
hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia
Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao.
Hali
hiyo inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa
waraghabishi na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji hicho akiwemo
Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa
kitongoji cha Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa ujasiri na elimu ya uraia
wananchi wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.
Kwa
mujibu wa bi Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha
Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo Blog
alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji aliweza kutoa hamasa kwa
wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu
uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki kupiga
kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki
katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano
ya kijiji.
Wengi
wa wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza
kupata mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki
zao na kuwa na uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho
ambapo mwanzoni walikuwa hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi
hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta
za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha wanakijiji wenzao haki
na wajibu wao kwa nafasi kubwa .
“Viongozi
wa kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika
kwa kijiji hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza
kuhoji tulikosa ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona
umuhimu wa kushirikishwa” alinukuliwa bw. Boniface Izengo mmoja wa
waraghabishi wa kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari
hii.
Katika
hatua nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki bi Matilda Peter
amekuwa ni mmoja wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi
rika ambapo hukutana na vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na
sekondari na kuwajuza kuhusu mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri
jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.
Maazimio
yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na
maeneo mengine bila shughuli maalum kuwajibishwa na pia kuweza
kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji hicho ikiwemo
kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo
Pia
mkutano wa kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza
kujadiliwa kwa uwazi na pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo
kijijini kuwezesha wananchi hao kuweza kusoma na kuelewa kila
kinachoendelea kijijini kwao katika swala la maendeleo ya uchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni