HALMASHAURI ya wilaya ya Longido,mkoani Arusha, imefanikiwa
kuvunja ndoa bubu na kuwarejesha wanafunzi wawili wa shule ya msingi
walioachishwa shule na kuolewa na kuwarejesha shuleni na kuendelea na masomo
yao mwaka 2015 .
Afisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Shaaban
Shemzighwa, ameyaeleza hayo kwenye kikao cha elimu cha mkoa kilichokuwa
kikipitisha majina ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi mwaka 2015,ambao
wamechaguliwa kujiunga na sekondari mwakani .
Akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe ambao walitaka kufahamu
mkakati wa halmashauri hiyo kukabiliana na utoro unaosababsha wanafunzi
hasa wasichana ambao wamekuwa wakiacha
shule na kuolewa ,amesema halmashauri inaendelea na kuwarejesha wanafunzi wote
waliotoroka na kuolewa.
Amesema wanafunzi wawili ambao walikuwa wameolewa
wamerejeshwa kuendelea na masomo yao katika shule ya msingi Kitumbeine na lengo
ni kukabiliana na utoro wa wanafunzi.
Amesema licha ya utoro huo wa wanafunzi bado halmashauri
hiyo ya Longido, imezidi kaulisha wanafunzi wengi ukilinganisha na halmashauri
zingine za mkoa wa Arusha na hayo ni mafanikio makubwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Ernest Kahindi,
akichangia kwenye kikao hicho amesema watoto wa jamii za wafugaji waishio maeneo
yote ya mpaka na nchi ya Kenya, wanasoma shule za Kenya.
Amesema watoto wa jamii za wafugaji kusoma nchini Kenya ni
jambo la kawaida na lbda inachangiwa na jamii hizo kutokuishi karibu na
shule hivyo inakuwa ni rahisi kuwapeleka
nchini humo kusoma.
Amesema jiografia ya wilaya za mipakani hasa kwenye jamii za
wafugaji nayo ni tatizo maeneo mengi hayana bara bara, mawasiliano ,shule wala
miundo mbinu na matokeo yake ni kuwepo
na mahudhurio hafifu shuleni.
Amesema wakati wa likizo watoto hao hupelekwa nchini Kenya
ambako huwa baadhi yao wanaolewa na hilo ni njambo la kawaida kwa jamii za
wafugaji waishio mipakani .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni