Katibu
Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza
na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua
mkutano wa siku moja wa baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Jeshi
la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto meza kuu ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo, kushoto ni Mwenyekiti wa
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza
hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo,
Jenita Ndone. Katika kikao hicho Abdulwakil aliwataka watumishi wa
wizara yake wafanye kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta mafanikio
ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati),
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (wapili kushoto),
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi
la Wizara hiyo, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo,
Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita
Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano
daima kabla ya Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika
Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga akimkaribisha mgeni rasmi ambaye
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuja
kuzungumza na wajumbe wa kikao hicho (hawapo pichani) kabla ya kufungua
rasmi kikao hicho. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
John Mngodo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mtoa
Mada wa Benki ya NMB, Faraja Kaziulaya akiwasilisha mada ya jinsi
wanavyotoa huduma zao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki
hiyo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (meza ya
mbele kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo wakiwa na
baadhi wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza
kwa makini mtoa Mada wa Benki ya NMB, Faraja Kaziulaya (hayupo pichani)
akiiwasilisha mada ya jinsi wanavyotoa huduma zao pamoja na bidhaa
mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo. Abdulwakil alifungua kikao cha
Baraza hilo na wajumbe walijadili masuala mbalimbali ya kuiendeleza
Wizara hiyo zaidi.
Mjumbe
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka
Zanzibar, Shemsa Said akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo
kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne
kushoto waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (watatu
kushoto waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la
wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ukonga jijini Dar es
Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni