Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30)
amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua
kwa kujinyonga.
Akizungumzia tukio hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema
tukio hilo la aina yake limetokea Desemba mwaka huu majira ya saa 7
mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.
Msangi amemtaja mwanamke
huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye
ameuwawa na mumewe kwa kukatwa kichwani .
Kamanda
Msangi amesema chanzo cha tukio
hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. Inadaiwa kuwa baada ya
tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita
100 kutoka nyumbani kwake.
Aidha
mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole
na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno kuwa
ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na
mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni