LUGHA YA KISWAHILI YAINGIA KATIKA REKODI YA DUNIA

ala1
Theresia Mmasy Afisa masoko kutoka kampuni ya ALAF iliyodhamini tuzo hizo akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akielezea tuzo za shindanio la kuandika riwaya za kiswahili zilizofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya hivi karibuni na watanzania kuibuka washindi katika vipengere mbalimbali.
ala2
Enock Maregesi mshindi wa uandishi wa riwaya ya Kiswahili ya Kolonia Santita riwaya iliyoshinda katika mashindano ya uandishi wa riwaya za Kiswahili yaliyofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya akipokea tuzo yake kutoka kwa Piyush Kanti Nath Meneja Huduma na Masoko wa ALAF kampuni iliyodhamini tuzo hizo , Katikati ni Vikrant Srvanstava Meneja Mauzo ALAF.

KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika.
Akizungumza na wa

andishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.
 

Washindi wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.
Walioshiriki katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.

Amesema kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.

Katika tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya ALAF ilidhamini tuzo hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.

Afisa Masoko wa Alaf,Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni