Ponnar, kijana
aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, katika hospitali ya
Apollo akizungumza na waandishi wa habari baada ya upandikizaji huo.
Ponnar,
kijana aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, akiwa
katika picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Apollo baada ya
upandikizaji. Aliyemkumbatia ni Mwenyekiti na Mwanzilishi wa hospitali
za ApolloDk. Prathap .C. Reddy.
Na Mwandishi Wetu,
Hospitali
za Apollo zimefanikiwa kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya
upandikizaji wa moyo na ini; hivyo kujiunga na timu ya hospitali chache
duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa aina yake.
Desemba
2015; Hospitali za Apollo ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa
huduma za afya, kwa mara nyingine zimeonyesha ubora wake wa uongozaji
kupitia kituo cha upandikizaji duniani kwa kufanikisha upasuaji wa
upandikizaji kwa mpigo wa ogani za moyo na ini kwa kijana mwenye umri
wa miaka 30 anayetokea Tiruchengode, Tamilnadu nchini India.
Tukio
hilo linalotambulika kitaalam kama en-Bloc CHLTni mfumo mgumu wa
upasuaji na haujawahi fanyika popote barani Asia. Kama ilivyoitwa na
chuo cha Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na kitaalam sana, ambao
ni vyema uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa wenye ujuzi”, ni hizo
hatua za CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni pekee.
Stori
hii ya Ndg. Ponnar, kijana mtulivu kutokea Tiruchengode, mji mdogo
kutokea wilaya ya Namakkal Tamilnadunchini India. Ponnar alikuwa ni
mwanafunzi bora aliyemaliza stashahada yake kwenye fani ya uhandisi na
alikuwa na medali ya dhahabu.
Katika
umri wa miaka 22, kama kijana mwenye malengo makubwa na matumaini ya
kufikia ndoto zake, Ponnar alianza kuhisi kujaa maji tumboni mwake,
upungufu wa pumzi na kujikuta rangi ya ngozi yake kuanza kuwa manjano.
Hii
ilitambulika kama kufeli kwa ini, iliyopelekea kufanyiwa kwa
upandikizaji wa ini, ambao familia yake ilikuwa tayari kwa kijana huyo
kufanyiwa hilo zoezi la upandikizwaji. Wakati alipofika kwa ajili ya
kufanyiwa upasuaji huo wa kupandikizwa ini, iligundulika kuwa Ponnar
anatatizo katika mfumo wa upumuaji unaoitwa kitaalam Ebsteins anomaly au
kufeli kwa upande wa kulia wa moyo katika kufanya kazi kwa usahihi
ambao ndio awali umeletea udhoofu katika ini.
Bahati
mbaya kujumuika kwa matatizo mawili kwa mpigo kulimfanya Ndg Ponnar
kutokuwa na njia mbadala yoyote mbali na kujumlisha upandikizaji wa ini
na moyo. Hii ni hatua ya upasuaji inayohusisha njia kuu mbili kwanza
ya kupitia kooni na kifuani (kwa ajili ya moyo) na kupitia tumboni (kwa
ajili ya ini) hivyo kufanya zoezi kuwa hatari sana.
Ponnar-
kwa utulivu na ukakamavu alijiandaa kupigania uhai wake mpaka mwisho.
Familia yake hasa dada yake ambaye alikuwa tumaini na nguzo kwake,
maamuzi ya kwamba watafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamwokoa
kijana wao, walimpelekea hospitali za Apollo, Chennai, India.
“kwa
tatizo la kuwa na moyo usiofanya kazi ipasavyo, kulikuwa na presha
kubwa upande wa nyuma wa ini iliyosababisha kuharikika kwa seli za ini
iliyopelekea udhoofu huo wa ini. Kwa kuongezea, timu ya upandikizaji wa
ogani walijadili uwezekano mkubwa wa uvujaji mwingi wa damu hasa kwa
kuwa ni upasuaji wa sehemu mbili kwa mpigo na pia uwezekano mkubwa wa
sumu kujikusanya kwenye ini, kuathiri moyo hasa kama ogani hizo mbili
zitapandikizwa tofauti tofauti” alisema ”Dk. Paul Ramesh, mshauri
mwandamizi wa upasuaji katika mfumo wa upumuaji kutoka hospitali za
Apollo, Chennai.
Upasuaji na upandikizaji wa moyo na ini unaweza fanyika kwa njia kuu tatu;
1. Kwanza
upandikizaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini pale mgonjwa
atapokuwa amepata nafuu kutokana na upasuaji wa kwanza.
2. Kwanza upandikizwaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini kama njia mbili tofauti ila kwa mpigo katika operesheni moja.
3. Upandikizwaji wa moyo na ini kwa pamoja, inafanyika kwa ogani zote kuchukuliwa kama moja na kupachikwa kwa pamoja kwa mpigo.
Ni
wale mabigwa tu kwenye ile timu ya upandikizwaji wa ogani kufanya kazi
pamoja kama timu moja na kuleta matumaini ya kufanikisha en-bloc
CHLT mfumo adimu sana kufanyika duniani.
”kwa
zaidi ya miongo ya ujuzi katika upandikizwaji wa ogani, imetuwezesha
kupata maarifa na utaalamu unaohitajika kufanya operesheni ngumu kama
hizi.
Mafanikio
yetu katika upandikizwaji wa moyo na ini yaliyopatikana yametupatia
msingi na uimara katika uendeshaji bora wa en-bloc CHLT kwa bara la
Asia. Najivunia sana kwa ajili ya Ponnar na familia yake walioweza
kuimanini timu kutoka hospitali yetu ya Apollo, imetupa sana motisha
sisi kuendelea mbele na mfumo huu bila mipaka ili kufika juu kabisa.
Aliongeza Dk. Ramesh.
Ponnar
alisubiri kutokea April hadi 0ktoba 2015 ili mtoaji damu anayemfaa
alipopatikana. Alifanyiwa upasuaji wa upandikizwaji huo wa moyo na ini
tarehe 14 oktoba 2015 na aliruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya wiki baada
ya upasuaji huo.
Leo
hii, Ponnar ni mzima wa afya njiani kuelekea kupona kabisa na kurudia
maisha yake ya awali- ni mwenye furaha sababu ngozi yake sio ya njano
tena, na sasa anaweza kuendelea kufurahia raha za maisha kama kutembea
kwa miguu yake mwenyewe. Kwa maumivu yaliyokuwa nyuma kwa miaka 8, sasa
Ponnar yupo huru kuendeleza matumaini yake na ndoto zake.
Ngazi
hii ya kimatibabu, ya upandikizwaji wa moyo na ini kwa mpigo (mara ya
kwanza barani Asia) ni hazina kubwa kwa Ndg Ponnar na dada
yake,walioweza kutosikiliza uzushi wa watu wote. Pia ni ushuhuda kuwa
timu ya madaktari wa upandikizwaji kutoka hospitali za Apollo Chennai
wamefanikiwa kufanya operesheni hii kwa mafanikio makubwa. Haya yote
yasingeweza kufanikiwa kama pia kusingekuwepo kwa ushirikiano mkubwa
kutoka serikali ya Tamilnadu na programu ya kujitolea ogani iliyopo
Tamilnadu ambayo imesifiwa ulimwenguni kwote kwa kazi kubwa walioifanya.
”mafaniko
haya makubwa ni agano kwa mabingwa wote wa upasuaji duniani, madaktari,
wataalam, manesi na wafanyakazi wote waliojitolea kuwahudumia wagonjwa
na kutoa huduma zilizopo katika viwango vya kimataifa. Upasuaji ni
matokeao ya mipango bora iliyofanywa kwa siku kadhaa kutoka kwa timu ya
wataalam upande wa moyo na ini na uonekanaji wa miundo mbinu bora na
wataalam waliokubuhu. Jitihada hizi shirikishi zinachukua timu zote za
upandikizaji ili kutathimini na kuweka mikakati kasha kuonyesha kuwa
fani hii ni ya kuheshimika”. Alisema Dk. Prathap C Reddy, mwenyekiti na
mwanzilishi wa Hospitali za Apollo
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali
ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho
imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta
huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma
bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya
kibinadamu".Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo
imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya
kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi
makubwa katika sekta ya afya nchini india.
Katika
safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka
nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya
upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000
za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha
idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na
zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india,
zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji
unaotumia mashine za kiroboti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni